Mwanamuziki David Adedeji Adeleke almaarufu Davido ingawa ni staa leo lakini ni bora kukumbuka zamani alikuwa mtoto kama sisi sote.

Habari Nyingine: Video ya Pasta Ng'ang'a akiwazaba makofi waumini wake yasambaa Marekani

Raia huyo wa Nigeria aliwakumbusha mashabiki wake alikotoka kwa picha za utotoni wakati bado ananyonya titi la mama yake.

Tofauti yake na wengi wetu ni kuwa, Davido alizaliwa katika familia tajiri ambapo baba yake mzazi Dkt. Adedeji Adeleke, ni mfanyabiashara maarufu na mwekezaji.

Habari Nyingine: Magazeti ya Kenya Jumanne, Septemba 24:Dadake Tob Cohen afichua sababu za kukosa mazishi ya nduguye

Katika nyingi ya picha hizo, mwanamuziki huyo anaonekana akiwa na marehemu mama yake aliyeaga dunia 2003 akiwa na umri wa miaka 40 kabla ya mwanawe kuinuka na kuwa staa mkubwa.

Habari Nyingine: Korti yamruhusu askofu kuvunja ndoa yake ya miaka 21 kwa kunyimwa tendo la ndoa

Davido ambaye umri wake ni miaka 27 na anayetarajia mtoto wa kiume kutoka kwa mpenzi wake kwa jina Chioma, alitaja mwonekano wake akiwa mtoto mdogo kuwa sawa na ule wa mabinti zake wawili, Imade na Hailey.

Habari Nyingine: Pasta Nga'ng'a kuwazaba makofi waumini wake na habari zingine zilizotamba sana

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZoNyg49mp6KbmJZ6u62MpquorJ9isaLCyJ2mZpmbnrmqutiopbKZXam2tbWMpZhmpZGirm7FwKScZrKRrK63wdOimGalkai1oq7IpKBnoKSiuQ%3D%3D